Al-A'raaf 7:9
الأعرافوَمَنْ خَفَّتْ مَوَٰزِينُهُۥ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓا۟ أَنفُسَهُم بِمَا كَانُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا يَظْلِمُونَ
Na yule ambaye vipimo vyake vitakuwa hafifu, basi hao ndio waliozihasirisha nafsi zao kwa sababu ya vile walivyokuwa wakizifanyia Ishara zetu udhalimu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na watakao kuwa na uzani khafifu, basi hao ndio walio zitia khasarani nafsi zao kwa sababu ya kuzipinga Ishara zetu. [9]
[9] Na wale ambao maovu yao yatakithiri kuliko mema yao, hao ndio watakuwa khasarani, kwa kuwa wameziuza nafsi zao kwa Shetani, wakaacha kuzingatia Ishara zetu kwa ukafiri na inda.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na yoyote yule ambaye mizani za vitendo vyake zitakuwa nyepesi, (kwa wingi wa maovu yake,) hao ndio waliopoteza bahati yao ya kupata radhi ya Allah Mtukufu, (Aliyetukuka,) kwa sababu ya kukiuka kwao mipaka kwa kuzikanusha aya za Allah Mtukufu, (Aliyetukuka,) na kukosa kuzifuata.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net