Al-A'raaf 7:8
الأعرافوَٱلْوَزْنُ يَوْمَئِذٍ ٱلْحَقُّ ۚ فَمَن ثَقُلَتْ مَوَٰزِينُهُۥ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْمُفْلِحُونَ
Na kipimo Siku hiyo kitakuwa kwa haki. Kwa hivyo, yule ambaye vipimo vyake vitakuwa vizito, basi hao ndio waliofaulu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Siku hiyo kipimo kitakuwa kwa Haki. Basi watakao kuwa na uzani mzito, hao ndio watakao fanikiwa. [8]
[8] Na Siku tutapo wauliza na kuwaeleza, vipimo vya vitendo vyao kwa ajili ya kulipwa vitakuwa vipimo vya uadilifu. Wale ambao mema yao yatazidi kuliko maovu yao watakuwa ndio wenye kufuzu, tutakao walinda na Moto na tutawatia Peponi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kuvipima vitendo vya watu Siku ya Kiyama kutakuwa ni kwa mizani ya kikweli, kwa usawa na uhaki ambao hauna maonevu. Basi yoyote yule ambaye mizani za vitendo vyake zitakuwa nzito, kwa wingi wa mema yake, hao ndio watakaofaulu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net