Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 7

Al-A'raaf 7:7

الأعراف

فَلَنَقُصَّنَّ عَلَيْهِم بِعِلْمٍ ۖ وَمَا كُنَّا غَآئِبِينَ

Maana

Tena hakika tutawasimulia kwa elimu. Wala Sisi si kwamba hatukuwepo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Tena tutawasimulia kwa ilimu; wala Sisi hatukuwa mbali . [7]

[7] Na tutawapa wote khabari ya kweli yote yaliyo kuwa kwao, kwa sababu hakika Sisi tumewadhibitia kila kitu chao, kwani Sisi hatukuwa mbali nao, wala hatukuwa hatujui waliyo kuwa wakiyafanya.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Tutawaelezea, tena tutawaelezea, viumbe wote yale waliyoyatenda, kutokana na ujuzi wetu wa vitendo vyao ulimwenguni katika yale tuliyowaamrisha na tuliyowakataza. Na wala Hatukuwa mbali na wao katika hali yoyote ile.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net