Al-A'raaf 7:6
الأعراففَلَنَسْـَٔلَنَّ ٱلَّذِينَ أُرْسِلَ إِلَيْهِمْ وَلَنَسْـَٔلَنَّ ٱلْمُرْسَلِينَ
Na hakika tutawauliza wale waliotumiwa Ujumbe, na pia hakika tutawauliza hao Wajumbe.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kwa yakini tutawauliza wale walio pelekewa Ujumbe, na pia tutawauliza hao Wajumbe. [6]
[6] Na Siku ya Kiyama hisabu ya Mwenyezi Mungu itachungua kila kitu kwa uadilifu. Tutawauliza watu tulio watumia Mitume: Je, Ujumbe umewafikilia? Na wamewajibu nini hao Wajumbe tulio watuma? Na tutawauliza Mitume pia: Je, mmefikisha yaliyo teremshwa kwenu kutoka kwa Mola wenu Mlezi? Na hao kaumu zenu wamekujibuni nini?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi tutawauliza, tena tutawauliza, wale watu waliopelekewa Mitume, «Mliwajibu vipi Mitume wetu?» Na tutawauliza, tene tutawauliza, wale Mitume kuhusu kuufikisha kwao ujumbe wa Mola wao na namna walivyojibiwa na wale watu waliotumwa kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net