Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 13

Al-A'raaf 7:13

الأعراف

قَالَ فَٱهْبِطْ مِنْهَا فَمَا يَكُونُ لَكَ أَن تَتَكَبَّرَ فِيهَا فَٱخْرُجْ إِنَّكَ مِنَ ٱلصَّـٰغِرِينَ

Maana

Akasema, "Basi teremka kutoka humo! Haikufalii kufanya kiburi humo. Basi toka! Hakika wewe ni miongoni mwa walio duni."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akasema: Basi teremka kutoka humo! Haikufalii kufanya kiburi humo. Basi toka! Hakika wewe u miongoni mwa walio duni. [13]

[13] Mwenyezi Mungu alimlipa kwa inda yake na kiburi chake kwa kumfukuza katika makao ya utukufu wake, na akamwambia: Teremka kutoka hapo baada ya kuwa katika pahala pa juu. Haikufalii ukapandwa kichwa na ukaasi humo! Toka huko, nawe umehukumiwa hizaya na udhalili!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Akasema kumwambia Iblisi, «Shuka kutoka Peponi, kwani haifai kwako kufanya ujeuri humo» toka Peponi, kwani wewe ni miongoni mwa wanyonge waliyo watwevu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net