Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 65 · Aya ya 7

At-Talaaq 65:7

الطلاق

لِيُنفِقْ ذُو سَعَةٍ مِّن سَعَتِهِۦ ۖ وَمَن قُدِرَ عَلَيْهِ رِزْقُهُۥ فَلْيُنفِقْ مِمَّآ ءَاتَىٰهُ ٱللَّهُ ۚ لَا يُكَلِّفُ ٱللَّهُ نَفْسًا إِلَّا مَآ ءَاتَىٰهَا ۚ سَيَجْعَلُ ٱللَّهُ بَعْدَ عُسْرٍ يُسْرًا

Maana

Mwenye wasaa atoe kiasi ya wasaa wake, na mwenye dhiki, atoe katika kile ambacho Mwenyezi Mungu alimpa. Mwenyezi Mungu hamjukumishi mtu ila kwa kiasi cha alichompa. Mwenyezi Mungu atajaalia baada ya dhiki faraja.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenye wasaa atoe kadiri ya wasaa wake, na mwenye dhiki atoe katika alicho mpa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu hamkalifishi mtu ila kwa kadiri ya alicho mpa. Mwenyezi Mungu atajaalia baada ya dhiki faraji. [7]

[7] Atoe mwenye nafasi nzuri ya riziki kwa mujibu alicho kunjuliwa na Mwenyezi Mungu, na mwenye dhiki ya pato atoe kwa kadiri alicho mpa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu hamkalifishi mtu ila kwa mujibu alicho mpa. Mwenyezi Mungu atajaalia baada ya dhiki faraji.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na atoe matumizi mume kulingana na kile alichojaaliwa na Allah Mtukufu kumpa mkewe aliyeachana naye, na amlipie mwanawe, iwapo mume ana uwezo wa kipato. Na yule aliyepungukiwa na kipato ambaye ni fukara, basi na atoe kulingana na kile alichopewa na Allah Mtukufu katika matumizi. Masikini halazimishwi kutoa kama kile anacholazimishwa tajiri. Allah Mtukufu Ataleta, baada ya dhiki na shida, ukunjufu wa maisha na kutosheka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Talaaq

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net