Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 65 · Aya ya 6

At-Talaaq 65:6

الطلاق

أَسْكِنُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ سَكَنتُم مِّن وُجْدِكُمْ وَلَا تُضَآرُّوهُنَّ لِتُضَيِّقُوا۟ عَلَيْهِنَّ ۚ وَإِن كُنَّ أُو۟لَـٰتِ حَمْلٍ فَأَنفِقُوا۟ عَلَيْهِنَّ حَتَّىٰ يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ ۚ فَإِنْ أَرْضَعْنَ لَكُمْ فَـَٔاتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ ۖ وَأْتَمِرُوا۟ بَيْنَكُم بِمَعْرُوفٍ ۖ وَإِن تَعَاسَرْتُمْ فَسَتُرْضِعُ لَهُۥٓ أُخْرَىٰ

Maana

Wawekeni humo humo mnamokaa nyinyi kwa kiasi cha pato lenu, wala msiwaletee madhara kwa kuwapa dhiki. Na wakiwa wana mimba, wagharimieni mpaka wajifungue. Na wakikunyonyesheeni, basi wapeni ujira wao, na shaurianeni kwa wema. Na mkiona uzito kati yenu, basi amnyonyeshee mwanamke mwingine.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wawekeni humo humo mnamo kaa nyinyi kwa kadiri ya pato lenu, wala msiwaletee madhara kwa kuwadhiki. Na wakiwa wana mimba, wagharimieni mpaka wajifungue. Na wakikunyonyesheeni, basi wapeni ujira wao, na shaurianeni kwa wema. Na mkiona uzito kati yenu, basi amnyonyeshee mwanamke mwengine. [6]

[6] Wawekeni wanawake waliomo edani humo humo katika nyumba zenu, kwa kadiri ya uwezo wenu. Wala msiwaletee madhara yoyote, kuwaletea dhiki katika maskani. Na ikiwa wana mimba basi watoleeni gharama za kuwakimu mpaka wazae. Wakikunyonyesheeni watoto wenu hao watalaka, basi wapeni ujira wao. Na amrishaneni mambo mazuri ya kusameheana na kuacha kutaabishana. Na ikitokea kati yenu dhiki na taabu, basi baba atafute mnyonyeshaji mwengine badala ya mama aliye achwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wakalisheni, wale walioachwa miongoni mwa wake zenu kwenye kipindi chao eda, mahali mfano wa pale mnapokaa nyinyi kwa kadiri ya uwezo wenu. Wala msiwafanyie mambo ya kuwadhuru mkawafanyia uzito katika makazi. Na iwapo wake zenu mliowapa talaka ni waja wazito, basi wapeni matumizi pindi wakiwa kwenye eda zao mpaka watakapozaa. Na iwapo watawanyonyeshea watoto wenu kwa malipo, basi wapeni malipo yao, na amrishaneni nyinyi kwa nyinyi wema na roho nzuri. Na iwapo hamkukubaliana juu ya unyonyeshaji wa mama mzazi, basi baba atanyonyeshewa na mnyonyeshaji mwingine asiyekuwa mama aliyepewa talaka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Talaaq

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net