At-Talaaq
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
لِيُنفِقْ ذُو سَعَةٍ مِّن سَعَتِهِۦ ۖ وَمَن قُدِرَ عَلَيْهِ رِزْقُهُۥ فَلْيُنفِقْ مِمَّآ ءَاتَىٰهُ ٱللَّهُ ۚ لَا يُكَلِّفُ ٱللَّهُ نَفْسًا إِلَّا مَآ ءَاتَىٰهَا ۚ سَيَجْعَلُ ٱللَّهُ بَعْدَ عُسْرٍ يُسْرًا 7
{7} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akaweka kipimo cha mali ya matumizi ya kila siku kulingana na hali ya mume, akasema: "Mwenye wasaa atoe kiasi ya wasaa wake." Yaani, tajiri na atoe kutoka katika utajiri wake, wala asitoe matumizi kama ya masikini. "Na mwenye dhiki, atoe katika kile ambacho Mwenyezi Mungu alimpa. Mwenyezi Mungu hamjukumishi mtu ila kwa kiasi cha alichompa." Haya yanafailiana na hekima ya Mwenyezi Mungu na rehema zake. Ambapo alimuamrisha kila mmoja kulingana na hali yake, na akamwepesishia mwenye uzito, na kwamba hamtwiki ila kile alichompa, sawa iwe ni katika mlango wa kutoa matumizi ya kila siku au mengineyo. "Mwenyezi Mungu atajaalia baada ya dhiki faraja." Hii ni bishara njema kwa wale walio katika matatizo kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaondolea dhiki na ugumu wake. Kwa maana pamoja na dhiki kuna wepesi. Hakika pamoja na dhiki kuna wepesi.