Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 65 · Aya ya 8

At-Talaaq 65:8

الطلاق

وَكَأَيِّن مِّن قَرْيَةٍ عَتَتْ عَنْ أَمْرِ رَبِّهَا وَرُسُلِهِۦ فَحَاسَبْنَـٰهَا حِسَابًا شَدِيدًا وَعَذَّبْنَـٰهَا عَذَابًا نُّكْرًا

Maana

Na miji mingapi iliyovunja amri ya Mola wake Mlezi na Mitume wake, basi tuliihisabia hisabu ngumu na tukaiadhibu kwa adhabu kali.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na miji mingapi iliyo vunja amri ya Mola wake Mlezi na Mitume wake, basi tuliihisabia hisabu ngumu na tukaiadhibu kwa adhabu kali. [8]

[8] Na miji mingi ambayo watu wake wamefanya ujabari na wakapuuza amri ya Mola wao Mlezi na Mitume wake, tukaihisabia kwa hisabu kali kwa kuchungua kila walilo litenda na kujadiliana nao, na tukawaadhibu adhabu ya kuchusha iliyo mbaya, wakagugumia malipo maovu ya mambo yao. Na ukawa mwisho wa mambo yao ni kukhasiri kukubwa mno.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kuna vitongoji vingi ambavyo watu wake waliasi amri ya Allah Mtukufu na amri ya Mitume Wake na wakaendelea kwenye ukiukaji wao na ukafiri wao, tukawahesabu juu ya matendo yao duniani hesabu kali mno na tukawaadhibu adhabu kubwa na mbaya.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Talaaq

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net