Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 65 · Aya ya 9

At-Talaaq 65:9

الطلاق

فَذَاقَتْ وَبَالَ أَمْرِهَا وَكَانَ عَـٰقِبَةُ أَمْرِهَا خُسْرًا

Maana

Basi ikauonja ubaya wa mambo yake; na mwisho wa mambo yao ilikuwa hasara.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi ikauonja ubaya wa mambo yake; na mwisho wa mambo yao ilikuwa khasara. [9]

[9] Wakagugumia malipo maovu ya mambo yao. Na ukawa mwisho wa mambo yao ni kukhasiri kukubwa mno.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wakauonja mwisho mbaya wa ujeuri wao na ukafiri wao, na mwisho wa ukafiri wao ulikuwa ni maangamivu na hasara, hapana hasara nyingine baada ya hiyo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Talaaq

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net