At-Talaaq 65:10
الطلاقأَعَدَّ ٱللَّهُ لَهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا ۖ فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ يَـٰٓأُو۟لِى ٱلْأَلْبَـٰبِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ۚ قَدْ أَنزَلَ ٱللَّهُ إِلَيْكُمْ ذِكْرًا
Mwenyezi Mungu aliwaandalia adhabu kali. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, enyi wenye akili, mlioamini! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteremshieni Ukumbusho.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwenyezi Mungu aliwaandalia adhabu kali. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, enyi wenye akili, mlio amini! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteremshieni Ukumbusho, [10]
[10] Mwenyezi Mungu amewaandalia watu wa miji ya watu walio fanya ujabari adhabu ya mwisho wa ukali. Basi tahadharini na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, enyi wenye akili sawa, ambao mnasifika kwa Imani. Amekuteremshieni mtu mwenye utukufu na cheo,
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Amewaandalia watu hawa, waliokiuka mipaka na wakaenda kinyume na amri za Allah Mtukufu na amri za Mitume Wake, adhabu kali sana. Basi muogopeni Allah Mtukufu na mjihadhari na mambo Anayoyachukia, (enyi watu wenye akili zilizokomaa), mliomuamini Allah Mtukufu na Mitume Wake na mkazifuata Sheria Zake kivitendo! Kwa hakika Allah Mtukufu Ameteremsha kwenu, (enyi Waumini), Ukumbusho wa kuwakumbusha nao na kuwazindusha juu ya fungu lenu la kumuamini Allah Mtukufu na kuwa watiifu Kwake kivitendo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net