Al-Jumu'a 62:4
الجمعةذَٰلِكَ فَضْلُ ٱللَّهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَآءُ ۚ وَٱللَّهُ ذُو ٱلْفَضْلِ ٱلْعَظِيمِ
Hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu anayompa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu anayo mpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa. [4]
[4] Kuletwa Mtume huko ni fadhila inayo toka kwa Mwenyezi Mungu. Anamkirimu kwayo aliye mkhitari katika waja wake. Na Mwenyezi Mungu peke yake, ndiye Mwenye fadhila kubwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
kutumwa huko kwa Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), kwa ummah wa Kiarabu na wasiokuwa wao, ni wema kutoka kwa Allah Mtukufu, humpa Anayemtaka miongoni mwa waja Wake. Na Yeye, Peke Yake, Ndiye Mwenye wema na upaji mwingi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net