Al-Jumu'a 62:3
الجمعةوَءَاخَرِينَ مِنْهُمْ لَمَّا يَلْحَقُوا۟ بِهِمْ ۚ وَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ
Na kwa wengine ambao bado hawajaungana nao. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kwa wengine ambao bado hawajaungana nao. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima. [3]
[3] Na pia Mwenyezi Mungu amempeleka Muhammad kwa watu wenginewe, ambao hawajaja bado, lakini watakuja. Na Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mwenye kushinda kila kitu, Mwenye hikima ya kufikia ukomo katika vitendo vyake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Amemtuma huyu mtume kwa watu wengine pia watakaokuja miongoni mwa Waarabu na wengineo. Na Allah Mtukufu Aliyetukuka, Peke Yake, Ndiye Mshindi mwenye kushinda juu ya kila kitu, Mwingi wa hekima katika maneno Yake na matendo Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net