Al-Jumu'a 62:2
الجمعةهُوَ ٱلَّذِى بَعَثَ فِى ٱلْأُمِّيِّـۧنَ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُوا۟ عَلَيْهِمْ ءَايَـٰتِهِۦ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ ٱلْكِتَـٰبَ وَٱلْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا۟ مِن قَبْلُ لَفِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ
Yeye ndiye aliyemtuma Mtume kwenye watu wasiojua kusoma na kuandika, awasomee Aya zake na awatakase, na awafunze Kitabu na hekima, ijapokuwa kabla ya haya walikuwa katika upotovu ulio dhahiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Yeye ndiye aliye mpeleka Mtume kwenye watu wasio jua kusoma, awasomee Aya zake na awatakase, na awafunze Kitabu na hikima, ijapo kuwa kabla ya haya walikuwa katika upotofu ulio dhaahiri. [2]
[2] Mwenyezi Mungu ndiye aliye mtuma Mtume kwa watu wasio jua kuandika, naye ni katika wao wenyewe, anawasomea Aya zake Mwenyezi Mungu, na anawasafisha na mambo machafu ya itikadi na tabia, na anawafundisha Qur'ani na kuijua Dini. Na wao kabla ya kuletwa yeye walikuwa wamepotoka kabisa kuiacha haki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu, kutakasika na kila upungufu ni Kwake, Ndiye Aliyetuma kwa Waarabu, wasiojua kusoma wala kuwa na kitabu wala kumbukumbu zozote za utume, Mtume aliyetokana na wao aliyetumwa kwa watu wote, awasomee Qur’ani, na awatakase na itikadi mbovu na tabia mbaya, na awafundishe Qur’ani na Sunnah. Na wao, kwa kweli, tangu alipokuwa hajatumwa mtume kwao, walikuwa kwenye ukengeukaji ulio wa wazi, kwa kuwa kando na haki. Na Allah Mtukufu, ametakasika na kila upungufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net