Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 62 · Aya ya 5

Al-Jumu'a 62:5

الجمعة

مَثَلُ ٱلَّذِينَ حُمِّلُوا۟ ٱلتَّوْرَىٰةَ ثُمَّ لَمْ يَحْمِلُوهَا كَمَثَلِ ٱلْحِمَارِ يَحْمِلُ أَسْفَارًۢا ۚ بِئْسَ مَثَلُ ٱلْقَوْمِ ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِ ٱللَّهِ ۚ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Maana

Mfano wa wale waliobebeshwa Taurati kisha wasiibebe, ni mfano wa punda anayebeba vitabu vikubwa vikubwa. Mfano muovu mno wa watu waliokadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhalimu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mfano wa walio bebeshwa Taurati kisha wasiibebe, ni mfano wa punda anaye beba vitabu vikubwa vikubwa. Mfano muovu mno wa watu walio kadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu. [5]

[5] Mfano wa Mayahudi walio funzwa Taurati, na wakalazimishwa waifuate, na wao hawakuifuata kwa vitendo, ni mfano wa punda aliye beba vitabu ambavyo hajui ndani yake mna nini. Ni mbaya mno mfano wa watu wanao kadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu hawasaidii kufikilia uwongofu watu ambao kazi yao ni kudhulumu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mfano wa Mayahudi ambao walitakiwa kuifuata Taurati kivitendo kisha wakakosa kuifuata ni kama mfano wa punda ambaye yuwabeba vitabu na hajui yaliyo ndani yake. Ni mfano muovu mno wa watu ambao wamezikataa aya za Allah Mtukufu na wasifaidike nazo. Na Allah Mtukufu Hawaelekezi kwenye wema watu madhalimu ambao wanaikiuka mipaka Yake na wanaotoka nje ya utiifu Kwake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Jumu'a

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net