Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 60 · Aya ya 5

Al-Mumtahana 60:5

الممتحنة

رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا فِتْنَةً لِّلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَٱغْفِرْ لَنَا رَبَّنَآ ۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ

Maana

Mola wetu Mlezi! Usitufanyie mtihani kwa waliokufuru. Na tusamehe, Mola wetu Mlezi. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mola wetu Mlezi! Usitufanyie mtihani kwa walio kufuru. Na tusamehe, Mola wetu Mlezi. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima. [5]

[5] Mola wetu Mlezi! Usitujaalie tukawa katika hali ya kuwa katika fitina za walio kufuru. Na tusamehe madhambi yetu, ewe Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu usiye shindika, Mwenye hikima katika kutasarafu kwake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mola wetu! Usitufanye ni mtihani wenye kuwanufaisha waliokukanusha, kwa kutuadhibu au kuwapa nguvu makafiri juu yetu, wakatufitini kwa kutuepusha na Dini yetu, au wakawa na nguvu juu yetu wakafitinika kwa hilo, na hapo waseme, «Lau hawa wangekua kwenye haki isingewapata adhabu hii,» na hapo wakazidisha ukafiri. Na utustirie dhambi zetu kwa kutusamehe, ewe Mola wetu! Hakika wewe ni Mshindi Asiyekuwa na mwenye kushindana Naye, Mwingi wa hekima katika maneno Yake na matendo Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Mumtahana

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net