Al-Mumtahana 60:4
الممتحنةقَدْ كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ فِىٓ إِبْرَٰهِيمَ وَٱلَّذِينَ مَعَهُۥٓ إِذْ قَالُوا۟ لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَءَٰٓؤُا۟ مِنكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ ٱلْعَدَٰوَةُ وَٱلْبَغْضَآءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤْمِنُوا۟ بِٱللَّهِ وَحْدَهُۥٓ إِلَّا قَوْلَ إِبْرَٰهِيمَ لِأَبِيهِ لَأَسْتَغْفِرَنَّ لَكَ وَمَآ أَمْلِكُ لَكَ مِنَ ٱللَّهِ مِن شَىْءٍ ۖ رَّبَّنَا عَلَيْكَ تَوَكَّلْنَا وَإِلَيْكَ أَنَبْنَا وَإِلَيْكَ ٱلْمَصِيرُ
Hakika nyinyi mna mfano mzuri kwenu kwa Ibrahim na wale waliokuwa pamoja naye, walipowaambia watu wao: Hakika sisi tumejitenga nanyi na hayo mnayoyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Tunakukataeni; na umekwisha dhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi mpaka mtakapomuamini Mwenyezi Mungu peke yake. Isipokuwa kauli ya Ibrahim kumwambia baba yake: Hakika nitakuombea msamaha, wala similiki chochote kwa ajili yako mbele ya Mwenyezi Mungu. Mola wetu Mlezi! Juu yako tumetegemea, na kwako tumeelekea, na kwako ndiyo marejeo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika nyinyi mna mfano mzuri kwenu kwa Ibrahim na wale walio kuwa pamoja naye, walipo waambia watu wao: Hakika sisi tumejitenga nanyi na hayo mnayo yaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Tunakukataeni; na umekwisha dhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi mpaka mtakapo muamini Mwenyezi Mungu peke yake. Isipo kuwa kauli ya Ibrahim kumwambia baba yake: Hakika nitakuombea msamaha, wala similiki chochote kwa ajili yako mbele ya Mwenyezi Mungu. Mola wetu Mlezi! Juu yako tumetegemea, na kwako tumeelekea, na kwako ndio marejeo. [4]
[4] Nyinyi mna kiigizo kizuri cha kukiiga katika Ibrahim na walio amini pamoja naye, pale walipo waambia watu wao: Hakika sisi tunajitenga nanyi, na tunajitenga na hiyo miungu ya uwongo mnayo iabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Sisi tunakukataeni, na umekwisha dhihiri uadui na kuchukiana baina yetu na nyinyi. Hayo hayataondoka kabisa mpaka mumuamini Mwenyezi Mungu peke yake. Lakini kauli ya Ibrahim kumwambia baba yake: Nitakutakia maghfira, na similiki kwa Mwenyezi Mungu kitu chochote - kauli hiyo si ya kufuatwa. Kwani hayo yalikuwa kabla hajajua huyo baba yake kashikilia kuwa adui wa Mwenyezi Mungu wala hageuki. Ilipo dhihiri kwake kuwa hakika huyo ni adui wa Mwenyezi Mungu alijitenga naye. Enyi waumini! Semeni: Mola wetu Mlezi! Kwako Wewe ndio tunategemea, na kwako Wewe tunarejea, na kwako Wewe ndio mwisho wetu Akhera.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa hakika mlikuwa na kiigizo kizuri, (enyi Waumini), kwa Ibrãhîm na wale waliokuwa pamoja naye waliposema kuwaambia wakanushaji Allah Mtukufu, «Sisi tumejiepusha na nyinyi na vile mnavyoviabudu kinyume na Allah Mtukufu. Tumewakanusha nyinyi na tumeukataa ukafiri mlionao, na umejitokeza nje uadui na machukivu ya milele baina yetu sisi na nyinyi madamu bado mko kwenye ukanushaji wenu, mpaka mmuamini Allah Mtukufu Peke Yake.» Lakini haliingii kwenye kuigiza tendo la Ibrãhîm la kumuombea msamaha baba yake, kwa kuwa hilo lilitokea kabla ya Ibrãhîm kudhihirikiwa kuwa baba yake ni adui wa Allah Mtukufu, na alipodhihirikiwa kuwa yeye ni adui wa Allah Mtukufu alijiepusha naye. Mola wetu! Kwako wewe tumetegemea, na kwako wewe tumerejea kwa kutubia, na kwako wewe ndiko marejeo Siku ya Kiyama.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net