Al-Mumtahana 60:3
الممتحنةلَن تَنفَعَكُمْ أَرْحَامُكُمْ وَلَآ أَوْلَـٰدُكُمْ ۚ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ يَفْصِلُ بَيْنَكُمْ ۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ
Hawatakufaeni jamaa zenu, wala watoto wenu Siku ya Kiyama. Mwenyezi Mungu atapambanua baina yenu, na Mwenyezi Mungu anayaona mno mnayoyatenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hawatakufaeni jamaa zenu, wala watoto wenu Siku ya Kiyama. Mwenyezi Mungu atapambanua baina yenu, na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda. [3]
[3] Hawatakufaeni kitu jamaa zenu wala watoto wenu mlio wafanya kuwa ni marafiki, na hali wao ni adui wa Mwenyezi Mungu na adui zenu. Katika Siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu atakutengeni mbali mbali. Atawatia maadui zake Motoni na marafiki zake Peponi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona yote myatendayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hawatawanufaisha jamaa zenu wa karibu wala watoto wenu kitu chochote mnapofanya urafiki na wakanushaji kwa ajili yao. Siku ya Kiyama Allah Mtukufu Atawatenganisha nyinyi na wao, Awatie Peponi wanaomtii na Awatie Motoni wanaomuasi. Na Allah Mtukufu Anayaona mnayoyafanya, hakuna chochote kinachofichika Kwake cha maneno yenu na matendo yenu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net