Al-Mumtahana 60:6
الممتحنةلَقَدْ كَانَ لَكُمْ فِيهِمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُوا۟ ٱللَّهَ وَٱلْيَوْمَ ٱلْـَٔاخِرَ ۚ وَمَن يَتَوَلَّ فَإِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلْغَنِىُّ ٱلْحَمِيدُ
Kwa yakini umekuwa mfano mzuri kwenu katika mwendo wao, kwa anayemtarajia Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na mwenye kugeuka, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha, Msifiwa mno.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwa yakini umekuwa mfano mzuri kwenu katika mwendo wao, kwa anaye mtarajia Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na mwenye kugeuka basi hakika Mwnyezi Mungu ni Mwenye kujitosha, Msifiwa. [6]
[6] Enyi Waumini! Bila ya shaka katika Ibrahim na walio kuwa pamoja naye, kipo kiigizo kizuri kwenu kwa vile walivyo wafanyia uadui maadui wa Mwenyezi Mungu. Kiigizo hicho ni kwa mwenye kutaraji kukutana na Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na mwenye kupuuza kufuata haya basi kajidhulumu nafsi yake. Kwani hakika Mwenyezi Mungu si mhitaji wa mwenginewe. Yeye ni Mwenye kustahiki peke yake sifa zote njema.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa hakika mlikuwa, (enyi Waumini), na kiigizo chema kwa Ibrãhîm, amani imshukie, na wale waliokuwa naye, kwa anayetumai kupata kheri kutoka kwa Allah Mtukufu duniani na Akhera. Na yoyote anayeyapuuza yale ambayo Allah Mtukufu Anamuitia nayo ya kuwaiga Manabii Wake na akafanya urafiki na maadui Wake, basi Allah Mtukufu Ndiye Mkwasi wa kutowahitajia waja Wake, Ndiye Mwenye kuhimidiwa kwa dhati Yake na sifa Zake, Ndiye Mwenye kushukuriwa kwa namna zote.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net