Al-Mumtahana 60:7
الممتحنةعَسَى ٱللَّهُ أَن يَجْعَلَ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَ ٱلَّذِينَ عَادَيْتُم مِّنْهُم مَّوَدَّةً ۚ وَٱللَّهُ قَدِيرٌ ۚ وَٱللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
Asaa Mwenyezi Mungu akatia mapenzi baina yenu na hao maadui zenu, na Mwenyezi Mungu ni Mweza, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe zaidi, Mwenye kurehemu mno.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Asaa Mwenyezi Mungu akatia mapenzi baina yenu na hao maadui zenu, na Mwenyezi Mungu ni Mweza, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. [7]
[7] Asaa Mwenyezi Mungu akajaalia yawepo mapenzi baina yenu na hao makafiri walio ni maadui zenu, kwa kuwapa tawfiki, kuwawezesha, kuingia katika Imani. Na Mwenyezi Mungu ana uweza ulio timia, ni Mkunjufu wa maghfira kwa mwenye kutubu, ni Mwenye kuwarehemu waja wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Huenda Allah Mtukufu Akaweka baina yenu, (enyi Waumini), na wale jamaa zenu washirikina, ambao mlikuwa na uadui nao, mapenzi baada ya machukivu na uwadui kwa kuvifanya vifua vyao viukubali Uislamu. Na Allah Mtukufu ni Muweza wa kila kitu, na Allah Mtukufu ni Mwingi wa msamaha kwa waja Wake, ni Mwingi wa huruma Kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net