Al-Mumtahana
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
عَسَى ٱللَّهُ أَن يَجْعَلَ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَ ٱلَّذِينَ عَادَيْتُم مِّنْهُم مَّوَدَّةً ۚ وَٱللَّهُ قَدِيرٌ ۚ وَٱللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ 7
{7} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kwamba uadui huu ambao [Mwenyezi Mungu] aliwaamrisha Waumini kwa washirikina na akawaelezea kuyafanya hivyo, kwamba hilo ni maadamu wanaendelea na ushirikina na ukafiri wao, na kwamba wakihamia imani, basi hakika hukumu inazunguka pamoja na sababu zake, na mapenzi ya kiimani yatarudi. Basi msikate tamaa, enyi waumini, ya kurudi kwao kwenye imani. “Asaa Mwenyezi Mungu akatia mapenzi baina yenu na hao maadui zenu” kwa kurejea kwao katika Imani. “na Mwenyezi Mungu ni Mweza” juu ya kila kitu. Na katika hilo ni kuziongoa nyoyo na kuzigeuza kutoka katika hali moja kwenda nyengine. “na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe zaidi, Mwenye kurehemu mno.” Hakuna dhambi isiyoweza kusamehewa naye, na wala hakuna aibu asiyoweza kuisitiri. “Sema: Enyi waja wangu waliojidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe mno, Mwenye kurehemuzaidi.” Katika Aya hii kuna ishara na habari njema ya kusilimu kwa baadhi ya washirikina, waliokuwa maadui wa waumini wakati huo. Na hayo yalikwisha tokea, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu.