Al-Mumtahana
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا فِتْنَةً لِّلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَٱغْفِرْ لَنَا رَبَّنَآ ۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ 5
{5} “Mola wetu Mlezi! Usitufanyie mtihani kwa waliokufuru.” Yaani, usiwape mamlaka juu yetu kwa sababu ya madhambi yetu, wakatutia majaribuni na wakatuzuia kufanya yale wanayoweza kutuzuia miongoni mwa mambo ya imani, na wao pia wakajiingiza majaribuni. Kwa maana ikiwa wataona kwamba wana mkono wa juu, watadhani kwamba wako kwenye haki, nasi tuko katika batili, basi wakazidisha ukafiri na kuvuka mipaka. “Mola wetu Mlezi. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu,” Mshindi wa kila kitu. “Mwenye hekima” anayeweka vitu mahali pake. Kwa nguvu zako na hekima yako, tupe ushindi dhidi ya maadui zetu, utusamehe madhambi yetu, na urekebishe kosoro zetu.