Al-An'aam 6:97
الأنعاموَهُوَ ٱلَّذِى جَعَلَ لَكُمُ ٱلنُّجُومَ لِتَهْتَدُوا۟ بِهَا فِى ظُلُمَـٰتِ ٱلْبَرِّ وَٱلْبَحْرِ ۗ قَدْ فَصَّلْنَا ٱلْـَٔايَـٰتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ
Na Yeye ndiye aliyewawekea nyota ili mwongoke kwazo katika giza mbalimbali za bara na bahari. Hakika tumezieleza kwa kina Ishara hizi kwa kaumu wanaojua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Yeye ndiye aliye kuwekeeni nyota ili mwongoke kwazo katika kiza cha bara na bahari. Hakika tumezichambua Ishara hizi kwa watu wanao jua. [97]
[97] Yeye ndiye aliye kufanyieni nyota zikuongozeni kwa zilivyo pangwa mfike mwendako, nanyi mnakwenda kizani usiku, bara au baharini. Hakika Sisi tumezibainisha dalili za rehema yetu, na uwezo wetu, kwa ajili ya watu ambao wanao nufaika kwa ilimu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Aliyewawekea, enyi watu, nyota ni alama ya nyinyi kujua njia kipindi cha usiku mnapopotea kwa sababu ya giza lingi, barani na baharini. Tumezifafanua hoja zilizo wazi, ili wazizingatie miongoni mwenu wenye elimu ya kumjua Allah Mtukufu na sheria Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net