Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 96

Al-An'aam 6:96

الأنعام

فَالِقُ ٱلْإِصْبَاحِ وَجَعَلَ ٱلَّيْلَ سَكَنًا وَٱلشَّمْسَ وَٱلْقَمَرَ حُسْبَانًا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ ٱلْعَزِيزِ ٱلْعَلِيمِ

Maana

Ndiye anayepambaza mwangaza wa asubuhi; na ameufanya usiku kuwa mapumziko, na jua na mwezi kwenda kwa hesabu. Hayo ndiyo makadirio ya Mwenye nguvu kubwa, Mwenye kujua yote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ndiye anaye pambazua mwangaza wa asubuhi; na ameufanya usiku kwa mapumziko na utulivu, na jua na mwezi kwenda kwa hisabu. Hayo ndiyo makadirio ya Aliye tukuka Mwenye nguvu, Mwenye ujuzi. [96]

[96] Ni Yeye ndiye anaye toa mwangaza wa mchana kutokana na giza- giza la asubuhi, ili vilivyo hai viende kupata njia za maisha yao. Na akaufanya usiku uwe ni wa mapumziko ya mwili na roho, na akaufanya mwendo wa jua na mwezi wende kwa mpango mzuri kabisa ili watu wajue nyakati za ibada zao na maisha yao. Huo ndio mpango ulio fanywa kwa hikima, ndio tadbiri ya Mwenye uwezo Mwenye kuumiliki ulimwengu, Mwenye kukusanya kila kitu katika ujuzi wake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Ndiye Ambaye Alipasua mwangaza wa asubuhi kutoka kwenye giza la usiku, na Akaufanya usiku ni wakati wa utulivu, anatulia humo anayechoka mchana na kupata fungu lake la mapumziko, na Akalifanya jua na mwezi zinatembea katika njia zake kwa hesabu ya sawasawa iliyokadiriwa, haibadiliki wala haigongani. Hayo ndiyo makadirio ya Al-’Azîz, Mwenye kushinda, ambaye ufalme Wake umeshinda, Al-’Alîm, Aliye Mjuzi wa maslahi ya viumbe Wake na kuendesha mambo yao. Al- ’Azîz na Al-’Alîm ni miongoni mwa majina ya Allah Mtukufu mazuri yanayoonesha ukamilifu wa ushindi na ujuzi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net