Al-An'aam
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
فَالِقُ ٱلْإِصْبَاحِ وَجَعَلَ ٱلَّيْلَ سَكَنًا وَٱلشَّمْسَ وَٱلْقَمَرَ حُسْبَانًا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ ٱلْعَزِيزِ ٱلْعَلِيمِ 96
{96} Na Yeye Mtukufu alipotaja asili ya kuumbwa kwa vyakula, Akataja neema yake ya kutayarisha makazi, na kuumba kwake kila wanachokihitaji waja wake miongoni mwa mwangaza na giza; na yanayotokana na hayo miongoni mwa aina mbalimbali za manufaa na maslahi. Kwa hivyo Akasema, "Ndiye anayepambazua mwangaza wa asubuhi;" yaani, kama vile anavyopasua nafaka na kokwa. Vile vile Yeye ndiye mpasuaji wa giza la usiku totoro linaloenea kila kitu kilicho juu ya uso wa ardhi, kwa mwangaza wa asubuhi, ambao huipambazua kidogo kidogo, mpaka litoweke giza lote la usiku, na uje nyuma yake mwangaza na nuru ya jumla ambayo viumbe wanavitumia katika maslahi yao, na maisha yao, na manufaa yao ya kidini yao na dunia. Na kwa kuwa viumbe wanahitaji utulivu, na uthabiti, na mapumziko, ambavyo haviwezi kupatikana isipokuwa kwa kuwepo kwa mchana na mwangaza, mwenyezi Mungu "akaufanya" usiku kuwa mahali pa kupumzika, ambapo wandamu wanapumzikia katika nyumba zao, na katika kulala kwao. Nao mifugo katika mazizi yao, na ndege katika viota vyao, ili wapate fungu lao katika mapumziko. Kisha mwenyezi Mungu anaondoa hilo kwa mwangaza, na vivyo hivyo milele mpaka Siku ya Qiyama. "Na" Yeye mtukufu akalifanya "jua na mwezi kwenda kwa hesabu," ambapo kwa viwili hivyo zinajulikana zama na nyakati. Kwa hivyo, zinakuwa sawaswa nyakati za ibada kwa hilo, na tarehe za mwisho za miamala; inajulikana kwa hilo muda wa zama zilizopita. Na lau si kwa sababu ya kuwepo kwa jua na mwezi, na kupishana kwake, na kutofautiana kwake, basi watu wote hawangejua hayo, na wakawa sawa katika kuyajua. Bali hangeyajua isipokuwa watu fulani tu miongoni mwa watu, tena baada ya kujitahidi. Na kwa sababu ya hilo, yanapotea yale yangepotea miongoni mwa maslahi muhimu. "Hayo" makadirio yaliyotajwa ni "makadirio ya Mwenye nguvu kubwa, Mwenye kujua yote." Ambaye katika nguvu yake, vilifuata amri yake vitu hivi vikubwa, kwa hivyo vikakwenda kwa kunyenyekea, na kutiishwa kwa amri yake, kwa kiasi kwamba havipiti kile alichovipimia Mwenyezi Mungu, wala havitangulii kabla yake, wala havichelewi. Yeye ni Mwenye kujua ambaye kujua kwake kumeenea yote ya dhahiri na ya ndani, na ya mwanzo na ya mwisho. Na katika ushahidi wa kiakili juu ya kuenea kwa elimu ni kutiishwa kwa viumbe hivi vikubwa kwa makadirio na mpangilio wa ajabu unaoshangaza akili katika uzuri wake, na ukamilifu wake, na kuwiana kwake na masilahi na hekima.