Al-An'aam 6:95
الأنعامإِنَّ ٱللَّهَ فَالِقُ ٱلْحَبِّ وَٱلنَّوَىٰ ۖ يُخْرِجُ ٱلْحَىَّ مِنَ ٱلْمَيِّتِ وَمُخْرِجُ ٱلْمَيِّتِ مِنَ ٱلْحَىِّ ۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ
Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mpasuaji nafaka na mbegu za tende, zikachipua. Humtoa aliye hai kutokana na maiti, na humtoa maiti kutokana na aliye hai. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu. Basi vipi mnadanganywa?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mpasuaji mbegu na kokwa, zikachipua. Humtoa aliye hai kutoka maiti, naye ni mtoaji maiti kutokana na aliye hai. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu. Basi vipi mnageuzwa? [95]
[95] Hakika dalili za uwezo wa Mwenyezi Mungu kufufua, na kuwa ni Yeye pekee anaye stahiki kuabudiwa, na kufufua kwake watu kutoka makaburini, zimeenea na zimo za namna mbali mbali. Kwani ni Yeye peke yake ndiye anaye ipasua mbegu ukachipua mmea, na ni Yeye ndiye anaye ipasua kokwa ukatokeza mti. Na hivyo humfufua aliye hai kutokana na kisicho kuwa hai, kama mtu kutokana na udongo. Na akatoa kisicho kuwa hai kutokana na kilicho hai, kama maziwa kutokana na mnyama. Huyo Muweza Mtukufu ndiye Mungu wa Haki. Basi kisiwepo kitu cha kukugeuzeni mkaacha kumuabudu Yeye mkaviabudu vyenginevyo. Imeunganishwa Aya hii ya kupasua mbegu na kokwa, na Aya ya kupambazua asubuhi ambayo inaashiria kuwepo mwangaza, na kiza, na ya kwamba mwangaza umeshikamana kwa nguvu na kukua kwa mimea na miti. Hayo ni kwa kuwa mbegu na kokwa baada ya kuchipua zinahitajia chakula. Na chakula hichi kinatokana na mbolea maalumu kutokana na ardhi, na pia kutokana na mwangaza wa jua. Kwa hivyo mizizi yao inakwenda chini kutafuta chakula cha ardhi, na vigogo vyake na matawi inapata chakula kutokana na mwako wa jua ambalo ndilo linachomoza asubuhi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Anapasua mbegu ukatoka mmea, na Anapasua kokwa ukatoka mti. Anatoa chenye uhai kutokana na kilichokufa, kama vile binadamu na mnyama kutokana na tone la manii ya binadamu na mnyama. Na Anatoa kilichokufa kutokana na chenye uhai, kama tone la manii linalotokana na binadamu na mnyama. Huyo Ndiye Allah Mtukufu. Yaani Mwenye kufanya hili ni Allah Mtukufu, Peke Yake, Asiye na mshirika, Anayestahiki kuabudiwa. Basi vipi nyinyi mtaepushwa na haki mpelekwe kwenye batili mkamuabudu pamoja na Yeye mwingine asiyekuwa Yeye?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net