Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 94

Al-An'aam 6:94

الأنعام

وَلَقَدْ جِئْتُمُونَا فُرَٰدَىٰ كَمَا خَلَقْنَـٰكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَتَرَكْتُم مَّا خَوَّلْنَـٰكُمْ وَرَآءَ ظُهُورِكُمْ ۖ وَمَا نَرَىٰ مَعَكُمْ شُفَعَآءَكُمُ ٱلَّذِينَ زَعَمْتُمْ أَنَّهُمْ فِيكُمْ شُرَكَـٰٓؤُا۟ ۚ لَقَد تَّقَطَّعَ بَيْنَكُمْ وَضَلَّ عَنكُم مَّا كُنتُمْ تَزْعُمُونَ

Maana

Nanyi mlitujia wapweke kama tulivyowaumba mara ya kwanza. Na mkayaacha nyuma yenu yote tuliyowapa, na wala hatuwaoni hao waombezi wenu, ambao mlidai kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu kwenu. Yamekatika mahusiano baina yenu, na yamekupoteeni mliyokuwa mkiyadai.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Nanyi mlitujia wapweke kama tulivyo kuumbeni mara ya kwanza. Na mkayaacha nyuma yenu yote tuliyo kupeni, na wala hatuwaoni hao waombezi wenu, ambao mlidai kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu kwenu. Yamekatika makhusiano baina yenu, na yamekupoteeni mliyo kuwa mkidai. [94]

[94] Na Mwenyezi Mungu atawaambia Siku ya Kiyama: Sasa bila ya shaka mmekwisha yakinisha kwa nafsi zenu kuwa kweli mmefufuliwa kutoka makaburini kwenu, kama tulivyo kuumbeni mara ya kwanza. Na mmetujia hali ni wapweke, hamna mali, wala watoto, wala marafiki. Na mmeviacha nyuma yenu vyote tulivyo kupeni na mkaghurika navyo. Na wala Sisi hatuwaoni pamoja nanyi hao waombezi ambao mlidai kuwa watakunusuruni kwa Mwenyezi Mungu, na kuwa wao ati ni washirika wa Mwenyezi Mungu katika ibada! Makhusiano yote baina yenu na wao yamekwisha katika, na yamekupoteeni mliyo kuwa mkidai kuwa yatakufaeni.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika mmetujia ili muhesabiwe na mulipwe mkiwa peke yenu, kama tulivyowafanya mpatikane ulimwenguni mara ya kwanza mkiwa miguu mitupu, hamna nguo, mmeviacha nyuma yenu vitu ambavyo tuliwamakinisha navyo miongoni mwa mali ya ulimwenguni mliokuwa mkijigamba nayo. Na hatuwaoni masanamu wako na nyinyi Akhera ambao mlikuwa mkiitakidi kuwa watawaombea na mkidai kuwa ni washirika pamoja na Allah Mtukufu katika ibada. Mashikamano yaliyokuwa kati yenu ulimwenguni yameondoka, na yamewaondokea yale mliokuwa mkiyadai kwamba waungu wenu ni washirika wa Allah Mtukufu katika ibada, na imefunuka wazi kwamba nyinyi ndio mliopata hasara ya nafsi zenu, watu wenu na mali yenu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net