Al-An'aam 6:93
الأنعاموَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ ٱفْتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوْ قَالَ أُوحِىَ إِلَىَّ وَلَمْ يُوحَ إِلَيْهِ شَىْءٌ وَمَن قَالَ سَأُنزِلُ مِثْلَ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ ۗ وَلَوْ تَرَىٰٓ إِذِ ٱلظَّـٰلِمُونَ فِى غَمَرَٰتِ ٱلْمَوْتِ وَٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ بَاسِطُوٓا۟ أَيْدِيهِمْ أَخْرِجُوٓا۟ أَنفُسَكُمُ ۖ ٱلْيَوْمَ تُجْزَوْنَ عَذَابَ ٱلْهُونِ بِمَا كُنتُمْ تَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ غَيْرَ ٱلْحَقِّ وَكُنتُمْ عَنْ ءَايَـٰتِهِۦ تَسْتَكْبِرُونَ
Na ni nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia uongo Mwenyezi Mungu, au anayesema: 'Mimi nimeletewa wahyi'; na ilhali hakuletewa wahyi wowote. Na yule anayesema: Nitateremsha kama alivyoteremsha Mwenyezi Mungu. Na lau ungeliwaona madhalimu wanapokuwa katika mahangaiko ya mauti, na Malaika wamewanyooshea mikono wakiwambia: Zitoeni roho zenu! Leo mtalipwa adhabu ya kudunisha kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyasema juu ya Mwenyezi Mungu yasiyo ya haki, na mlivyokuwa mkizifanyia kiburi Ishara zake.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye mzuliya uwongo Mwenyezi Mungu, au anaye sema: Mimi nimeletewa wahyi; na hali hakuletewa wahyi wowote. Na yule anaye sema: Nitateremsha kama alivyo teremsha Mwenyezi Mungu. Na lau ungeli waona madhaalimu wanavyo kuwa katika mahangaiko ya mauti, na Malaika wamewanyooshea mikono wakiwambia: Zitoeni roho zenu! Leo mtalipwa adhabu ya fedheha kwa sababu ya mliyo kuwa mkiyasema juu ya Mwenyezi Mungu yasiyo ya haki, na mlivyo kuwa mkizifanyia kiburi Ishara zake. [93]
[93] Nabii huyu hakusema uwongo alipo tangaza kuwa Qur'ani imetoka kwaMwenyezi Mungu. Na hapana mwenye kumshinda kwa udhaalimu huyo aliye mzulia uwongo Mwenyezi Mungu, au akasema: Nimepata wahyi (ufunuo) kutoka kwa Mwenyezi Mungu, bila ya kuwa kapata wahyi wowote ule. Vile vile hapana dhaalimu mkubwa zaidi kuliko anaye sema: Mimi nitaleta maneno sawa na hayo aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu! Na lau kuwa unaijua hali ya hao madhaalimu nao wamo katika shida za mauti, na Malaika wanazing'oa roho zao kutokana na miili yao, kwa ukali na nguvu, ungeli ona vitisho vya kushitua vinawashukia! Wakati huo hao huambiwa: Sasa malipo yenu ya adhabu ya kudhalilisha na kufedhehesha yanaanza. Malipo haya ni kwa vile mlivyo kuwa mkimzulia Mwenyezi Mungu bila ya haki, na ni malipo kwa kuwa kiburi chenu kilikuzuieni msiangalie na kuzipima Aya, Ishara, za uumbaji za Mwenyezi Mungu ziliomo katika Qur'ani.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ni nani mbaya zaidi wa udhalimu kuliko yule aliyemzulia Allah Mtukufu, Aliyetukuka, neno la urongo, akadai kwamba Yeye Hakumtuma mjumbe yoyote miongoni mwa wanadamu, au akafanya madai ya urongo kwamba Allah Mtukufu Amemletea wahyi na hali hakumletea wahyi wowote, au akadai kwamba yeye ni muweza wa kuteremsha mfano wa Qur’ani Aliyoiteremsha Allah Mtukufu? Na lau wawaona hawa wenye kupita mpaka, nao wako kwenye vitisho vya kufa, ungaliona jambo la kufazaisha, huku Malaika wakizitwaa roho zao, wameikunjua mikono yao kwa adhabu, wanawaambia, «Zitoeni nafsi zenu. Leo mtadhalilishwa upeo wa kudhalilishwa, kama mlivyokuwa mkisema urongo juu ya Allah Mtukufu na mkiona kiburi kufuata aya Zake na kufuata Mitume Wake».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net