Al-An'aam 6:92
الأنعاموَهَـٰذَا كِتَـٰبٌ أَنزَلْنَـٰهُ مُبَارَكٌ مُّصَدِّقُ ٱلَّذِى بَيْنَ يَدَيْهِ وَلِتُنذِرَ أُمَّ ٱلْقُرَىٰ وَمَنْ حَوْلَهَا ۚ وَٱلَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِٱلْـَٔاخِرَةِ يُؤْمِنُونَ بِهِۦ ۖ وَهُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ
Na hiki ni Kitabu tulichokiteremsha, kilichobarikiwa, chenye kusadikisha yale yaliyokitangulia, na ili uuonye Mama wa Miji na wale walio pembezoni mwake. Na wale wanaoiamini Akhera wanakiamini, nao wanazihifadhi Swala zao.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hiki ni Kitabu tulicho kiteremsha, kilicho barikiwa, chenye kuhakikisha yaliyo tangulia, na ili uuwonye Mama wa Miji na walio pembezoni mwake. Na wenye kuamini Akhera wanakiamini hichi, nao wanazihifadhi Sala zao. [92]
[92] Na hii Qur'ani tumeiteremsha - kama tulivyo iteremsha Taurati - ina kheri nyingi, na itabaki mpaka Siku ya Kiyama. Inasadikisha Vitabu vilivyo teremshwa mbele yake, inaeleza khabari ya kuteremkwa kwao, ili iwape bishara Waumini, na iwakhofishe makafiri wa Makka na pembezoni mwake pande zote za dunia juu ya ghababu ya Mwenyezi Mungu, ikiwa hawakuifuata. Na wale wanao isadiki Siku ya malipo, kule kutaraji kwao thawabu na kukhofu adhabu, kunawapelekea kuiamini hii Qur'ani. Na kwa hivyo wao wanahifadhi kutekeleza Swala kwa ukamilifu na utimilivu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hii Qur’ani ni Kitabu tulichokuteremshia, chenye manufaa makubwa, kinatoa ushahidi juu ya ukweli wa vitabu vilivyoteremshwa vilivyokuja kabla yake na juu ya kwamba vinatoka kwa Allah Mtukufu. Tumekiteremsha ili uwatishie nayo, watu wa Makkah na walioko pambizoni mwake kwenye majimbo yote ya ardhi, adhabu ya Allah Mtukufu na mateso Yake. Na wenye kuamini uhai wa Akhera, wanaamini kwamba Qur’ani ni maneno ya Allah Mtukufu na wanajilazimisha kusimamisha Swala kwa nyakati zake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net