Al-An'aam 6:91
الأنعاموَمَا قَدَرُوا۟ ٱللَّهَ حَقَّ قَدْرِهِۦٓ إِذْ قَالُوا۟ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ عَلَىٰ بَشَرٍ مِّن شَىْءٍ ۗ قُلْ مَنْ أَنزَلَ ٱلْكِتَـٰبَ ٱلَّذِى جَآءَ بِهِۦ مُوسَىٰ نُورًا وَهُدًى لِّلنَّاسِ ۖ تَجْعَلُونَهُۥ قَرَاطِيسَ تُبْدُونَهَا وَتُخْفُونَ كَثِيرًا ۖ وَعُلِّمْتُم مَّا لَمْ تَعْلَمُوٓا۟ أَنتُمْ وَلَآ ءَابَآؤُكُمْ ۖ قُلِ ٱللَّهُ ۖ ثُمَّ ذَرْهُمْ فِى خَوْضِهِمْ يَلْعَبُونَ
Na hawakumkadiria Mwenyezi Mungu kwa haki ya kadri yake, waliposema: Mwenyezi Mungu hakumteremshia mwanaadamu chochote. Sema: Nani aliyekiteremsha Kitabu alichokuja nacho Musa, chenye nuru na uwongofu kwa watu, mlichokifanya kurasa kurasa mkizionyesha, na mengi mkiyaficha? Na mkafunzwa mliyokuwa hamyajui nyinyi wala baba zenu? Sema: 'Mwenyezi Mungu.' Kisha waache wacheze katika porojo lao.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hawakumkadiria Mwenyezi Mungu kwa haki ya kadri yake, walipo sema: Mwenyezi Mungu hakumteremshia mwanaadamu chochote. Sema: Nani aliyo teremsha Kitabu alicho kuja nacho Musa, chenye nuru na uwongofu kwa watu, mlicho kifanya kurasa kurasa mkizionyesha, na mengi mkiyaficha. Na mkafunzwa mlio kuwa hamyajui nyinyi wala baba zenu? Sema: Mwenyezi Mungu. Kisha waache wacheze katika porojo lao. [91]
[91] Na hawa makafiri hawakumkadiria Mwenyezi Mungu na rehema yake na hikima yake kwa anavyo stahiki, walipo kanya kuteremshwa ujumbe wake kwa binaadamu yeyote! Ewe Nabii! Waambie washirikina na wanao waunga mkono katika hayo miongoni mwa Mayahudi: Nani aliye kiteremsha Kitabu alicho kuja nacho Musa, ambacho kina nuru iliyo zagaa, na uwongofu wa kuongozea? Nyinyi Mayahudi mnakifanya hicho kuwa ni maandiko yaliyo gawiwa mafungu mbali mbali. Yanayo kubaliana na mapendo yenu mnayaonyesha, na mengi mnayaficha yale yanayo kupelekeeni kuiamini na kuisadiki Qur'ani. Na kutokana na Kitabu hicho mmejifunza mambo ambayo nyinyi na baba zenu hamkuwa mkiyajua!! Na ewe Nabii! Jawabu wape wewe kwa kuwaambia: Mwenyezi Mungu ndiye aliye iteremsha Taurati. Kisha waache wakiendelea katika upotovu, wakicheza kama watoto wadogo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hawa washirikina hawakumtukuza Allah Mtukufu ipasavyo kumtukuza, kwani walikanusha kwamba Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Amemteremshia yoyote miongoni mwa binadamu, chochote katika wahyi wake. Waambie, ewe Mtume, «Iwapo mambo ni kama mnavyodai, ni nani aliyeteremsha kitabu alichokuja nacho Mûsã kwa watu wake, kikiwa ni mwangaza kwa watu na mwongozo kwao?» Kisha maneno yakaelekea kwa Mayahudi kwa kuwakemea kwa kusema «Mnakigawanya kitabu hiki kwenye kurasa mbalimbali, nyingine mnazionesha na nyingi katika hizo mnazificha.- Kati ya hizo walizozificha ni maelezo ya sifa za Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, na unabii wake.- Pia Allah Mtukufu Aliwafundisha, nyinyi Waarabu, Qur’ani ambayo Aliiteremsha kwenu, ndani yake mna habari ya walio kabla yenu na walio baada yenu na yatakayokuwa baada ya kufa kwenu, habari ambazo hamkuwa mkizijuwa, nyinyi wala wazazi wenu.» Sema, «Allah Mtukufu Ndiye Aliyeiteremsha.» Kisha waache hawa wazame na kucheza katika mazungumzo yao ya ubatili.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net