Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 90

Al-An'aam 6:90

الأنعام

أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ هَدَى ٱللَّهُ ۖ فَبِهُدَىٰهُمُ ٱقْتَدِهْ ۗ قُل لَّآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا ۖ إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرَىٰ لِلْعَـٰلَمِينَ

Maana

Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewaongoa. Basi fuata uongofu wao. Sema: Mimi siwaombi ujira wowote juu yake. Haya si isipokuwa ni ukumbusho kwa walimwengu wote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewahidi. Basi fuata hidaya yao. Sema: Mimi sikuombeni ujira. Haya hayakuwa ila ni mawaidha kwa walimwengu wote. [90]

[90] Hao ndio Mwenyezi Mungu amewawezesha kuishika Njia ya Haki na kheri. Basi nyinyi wafuateni hao katika mambo waliyo wafikiana kwayo, nayo ni mambo ya misingi ya Dini, na misingi ya mwendo mwema, wala msifuate njia nyengine isiyo kuwa yao... Ewe Nabii! Waambie watu wako kama wao hawa walivyo waambia watu wao: Sitaki kwenu ujira kwa ajili ya kulifikisha Neno la Mwenyezi Mungu! Hii Qur'ani si chochote ila ni Ukumbusho kwa walimwengu wote, wala sina lengo mimi ila kuwa nyinyi mnafiike na hii Qur'ani.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Manabii hao waliotajwa ndio ambao Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Amewaongoza kwenye dini Yake ya haki. Basi fuata uongofu wao, ewe Muhammad, na andama njia yao. Waambie washirikina, Mimi sitaki kutoka kwenu, kwa kufikisha Uislamu, badala ya ulimwengu. Malipo yangu yako kwa Allah Mtukufu. Na Uislamu ni kuita watu wote kwenye njia iliyolingana sawa na ni ukumbusho kwenu na kwa kila aliyekuwa kama nyinyi, kati ya wale wanaoendelea kwenye batili; huenda nyinyi mkawaidhika nao mkanufaika.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net