Al-An'aam 6:89
الأنعامأُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ ءَاتَيْنَـٰهُمُ ٱلْكِتَـٰبَ وَٱلْحُكْمَ وَٱلنُّبُوَّةَ ۚ فَإِن يَكْفُرْ بِهَا هَـٰٓؤُلَآءِ فَقَدْ وَكَّلْنَا بِهَا قَوْمًا لَّيْسُوا۟ بِهَا بِكَـٰفِرِينَ
Hao ndio tuliowapa Kitabu, na hukumu, na Unabii. Kwa hivyo, ikiwa hawa (makafiri) watayakufuru, basi hakika tumekwishayawakilisha kwa kaumu wasioyakufuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hao ndio tulio wapa Vitabu na hukumu na Unabii. Ikiwa hawa watayakataa hayo, basi tumekwisha yawakilisha kwa watu wasio yakataa. [89]
[89] Hao ndio tulio wapa Vitabu vilivyo teremshwa, na ilimu zenye manufaa, na utukufu wa Unabii. Na washirikina wa Makka wakiyapinga mambo haya matatu, basi wamekwisha ahidiwa watu wengine wasiyo yakataa hayo wayachunge na wanafiike kwayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Manabii hao tuliowaneemesha kwa uongofu na unabii, ndio wale tuliowapa Kitabu, kama vile kurasa za Ibrãhîm, Taurati ya Mûsã, Zaburi ya Dãwûd na Injili ya ‘Ǐsâ. Na tuliwapa ufahamu wa Vitabu hivi na tukawateua kufikisha wahyi wetu. Na iwapo makafiri wa umma wako, ewe Mtume, watazikanusha aya za hii Qur’ani, basi tumewategemezea watu wengine jambo hilo, - yaani: Muhãjirûn (masahaba waliohamia Madina pamoja na Mtume) na Ans,ãr (masahaba wenyeji wa Madina) na wafuasi wao mpaka Siku ya Kiyama- ambao hawatakuwa ni wenye kuzikanusha. Bali watakuwa ni wenye kuziamini, ni wenye kuzitumia.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net