Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 88

Al-An'aam 6:88

الأنعام

ذَٰلِكَ هُدَى ٱللَّهِ يَهْدِى بِهِۦ مَن يَشَآءُ مِنْ عِبَادِهِۦ ۚ وَلَوْ أَشْرَكُوا۟ لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ

Maana

Huo ni uongofu wa Mwenyezi Mungu, anaongoa kwao amtakaye katika waja wake. Na lau wangelimshirikisha, basi yangeliwaharibikia yale waliyokuwa wakiyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hiyo ni hidaya ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo humhidi amtakaye katika waja wake. Na lau wangeli mshirikisha yangeli waharibikia waliyo kuwa wakiyatenda. [88]

[88] Hiyo ndiyo tawfiqi kubwa waliyo ipata watu hawa, nayo ni tawfiqi (uwezesho) iliyo tokana na Mwenyezi Mungu, ambayo humwafiqia (humwezesha) amtakaye katika waja wake. Na lau wangeli shiriki watu hawa walio khitariwa zingeli potea a'mali zao za kheri zote walizo zifanya, na wasingeli pata thawabu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Uongofu huo ni taufiki ya Allah Mtukufu ambayo kwayo Anamuongoza Anayemtaka miongoni mwa waja Wake. Na lau hawa Manabii wangemshirikisha Allah Mtukufu, kwa kuchukulia na kukadiria, amali zao zingeporomoka. Kwani Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Hakubali amali yoyote iliyoambatana na ushirikina.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net