Al-An'aam 6:87
الأنعاموَمِنْ ءَابَآئِهِمْ وَذُرِّيَّـٰتِهِمْ وَإِخْوَٰنِهِمْ ۖ وَٱجْتَبَيْنَـٰهُمْ وَهَدَيْنَـٰهُمْ إِلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ
Na katika baba zao, na vizazi vyao, na ndugu zao. Na tukawateua na tukawaongoa kwenye njia iliyonyooka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kutokana na baba zao, na vizazi vyao na ndugu zao. Na tukawateuwa na tukawaongoa kwenye Njia iliyo nyooka. [87]
[87] Na tuliwateuwa baadhi ya mababa wa hao, na dhuriya zao, na ndugu zao, na tukawakhitari wao, na tukawawezesha waifuate Njia isiyo kwenda upogo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na pia tuliwaongoza kwenye haki tuliowataka kuwaongoza kati ya wazazi wa hawa, watoto wao na ndugu zao. Na tuliwateua wao wafuate Dini yetu na wafikishe ujumbe wetu kwa wale tuliowatuma kwao. Na tuliwaonesha njia sahihi, isiyopotoka, nayo ni ile ya kumpwekesha Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na kumwepusha na mambo ya kumshirkisha.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net