Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 98

Al-An'aam 6:98

الأنعام

وَهُوَ ٱلَّذِىٓ أَنشَأَكُم مِّن نَّفْسٍ وَٰحِدَةٍ فَمُسْتَقَرٌّ وَمُسْتَوْدَعٌ ۗ قَدْ فَصَّلْنَا ٱلْـَٔايَـٰتِ لِقَوْمٍ يَفْقَهُونَ

Maana

Na Yeye ndiye aliyewaanzilisha kutokana na nafsi moja. Pako pahali pa kutulia na pa kupita njia. Hakika tumezichambua Ishara hizi kwa watu wanaofahamu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Yeye ndiye aliye kuzalisheni kutokana na nafsi moja. Pako pahali pa kutulia na pa kupita njia. Hakika tumezichambua Ishara hizi kwa watu wanao fahamu. [98]

[98] Yeye ndiye aliye kutoeni kwenye asli moja, nayo ni baba wa watu wote, Adam. Na Adam ametoka kwenye ardhi. Basi ardhi ndio kituo chenu muda wa uhai wenu, na ndipo pahala pa kupaaga baada ya kufa kwenu, na mkapotea chini yake. Na tumezibainisha dalili za uwezo wetu kwa watu wanao zingatia na kufahamu mambo yalivyo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Allah Mtukufu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Aliyeanza kuwaumba, enyi watu, kutokana na Ãdam, amani imshukie, Alipomuumba kwa udongo, kisha mkawa nyinyi ni kizazi chenye kuendelea kutokana na yeye, Akawafanyia kituo cha nyinyi kutulia, nacho ni zao za wanawake; na Akawafanyia hazina ya nyinyi kuhifadhiwa, nayo ni migongo ya wanaume. Tumeshawabainishia hoja na kuwapambanulia dalili na kuzithibitisha kwa watu wenye kufahamu vituo vya hoja na sehemu za mazingatio.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net