Al-An'aam 6:82
الأنعامٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَلَمْ يَلْبِسُوٓا۟ إِيمَـٰنَهُم بِظُلْمٍ أُو۟لَـٰٓئِكَ لَهُمُ ٱلْأَمْنُ وَهُم مُّهْتَدُونَ
Wale ambao waliamini, na hawakuchanganya imani yao na dhuluma, hao ndio wana amani, na wao ndio walioongoka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wale ambao wameamini, na hawakuchanganya imani yao na dhulma - hao ndio watakao pata amani na wao ndio walio ongoka. [82]
[82] Wanao muamini Allah, (Mwenyezi Mungu), na wasiichanganyishe imani yao hii na ibada ya yeyote asiye kuwa Yeye - hao tu ndio wenye haki ya kupata utulivu, na ni wao tu ndio walio ongoka kuishika Njia ya Haki na Kheri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wale waliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na wakafuata sheria Yake kivitendo, na wasichanganye imani yao na ushirikina, wao ndio wenye utulivu na usalama na wao ndio walioongozwa kwenye njia ya haki.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net