Al-An'aam 6:81
الأنعاموَكَيْفَ أَخَافُ مَآ أَشْرَكْتُمْ وَلَا تَخَافُونَ أَنَّكُمْ أَشْرَكْتُم بِٱللَّهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِۦ عَلَيْكُمْ سُلْطَـٰنًا ۚ فَأَىُّ ٱلْفَرِيقَيْنِ أَحَقُّ بِٱلْأَمْنِ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ
Na vipi nivihofu hivyo mlivyovishirikisha, ilhali nyinyi hamhofu kuwa nyinyi mmemshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu ambacho hakuwateremshia uthibitisho juu yake. Basi ni kundi gani katika mawili haya lina haki zaidi kupata amani, ikiwa nyinyi mnajua?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na vipi nivikhofu hivyo mnavyo vishirikisha, hali nyinyi hamkhofu kuwa nyinyi mmemshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu ambacho hakukiteremshia uthibitisho. Basi kundi gani katika mawili haya lina haki zaidi kupata amani, kama nyinyi mnajua? [81]
[81] Na katika ajabu ni kuwa mimi niiogope hiyo miungu yenu ya uwongo, na nyinyi hamna khofu kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu iliyo simama ushahidi wa Umoja wake, nyinyi mna shiriki kuabudu vitu ambavyo havina ushahidi kuwa vinastahiki kuabudiwa. Basi katika hali hii kikundi gani baina ya sisi chenye haki ya utulivu na amani, ikiwa kweli nyinyi mnaijua Haki na mnaitambua?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
«Na ni vipi nitaogopa masanamu yenu na hali nyinyi hamumuogopi Mola wangu Aliyewaumba na Akayaumba masanamu yenu ambayo mnamshirikisha nayo Allah Mtukufu katika ibada, bila ya kuwa na hoja yoyote juu ya hilo? Basi ni lipi kati ya makundi mawili, kundi la washirikina na kundi la wenye kumpwekesha Allah Mtukufu, lenye haki zaidi ya utulivu na usalama na kuaminika na adhabu ya Allah Mtukufu? Iwapo mnajua ukweli wa ninayoyasema, niambieni».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net