Al-An'aam 6:80
الأنعاموَحَآجَّهُۥ قَوْمُهُۥ ۚ قَالَ أَتُحَـٰٓجُّوٓنِّى فِى ٱللَّهِ وَقَدْ هَدَىٰنِ ۚ وَلَآ أَخَافُ مَا تُشْرِكُونَ بِهِۦٓ إِلَّآ أَن يَشَآءَ رَبِّى شَيْـًٔا ۗ وَسِعَ رَبِّى كُلَّ شَىْءٍ عِلْمًا ۗ أَفَلَا تَتَذَكَّرُونَ
Na kaumu yake wakamhoji. Akasema: Je, mnanihoji kuhusiana na Mwenyezi Mungu, na ilhali Yeye hakika amekwishaniongoa? Wala siogopi hao mnaowashirikisha naye, isipokuwa ikiwa Mola wangu Mlezi akipenda kitu. Mola wangu Mlezi amekusanya elimu ya kila kitu. Basi je, hamkumbuki?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na watu wake wakamhoji. Akasema: Je, mnanihoji juu ya Mwenyezi Mungu, na hali Yeye ameniongoa? Wala siogopi hao mnao washirikisha naye, ila Mola wangu Mlezi akipenda kitu. Mola wangu Mlezi amekusanya ilimu ya kila kitu. Basi je, hamkumbuki? [80]
[80] Na juu ya hivyo, watu wake walijadiliana naye katika Umoja wa Mwenyezi Mungu, na wakamtisha kuwa atapata ghadhabu ya miungu yao. Basi yeye akawaambia: Haikufaliini nyinyi kuzozana nami katika Umoja wa Mwenyezi Mungu, naye amekwisha nihidi kufikia Haki. Wala siogopi ghadhabu ya miungu yenu mnayo ifanya ni washirika wa Mwenyezi Mungu. Lakini Mola wangu Mlezi akipenda madhara yatatokea, kwa kuwa Yeye pekee ndiye Muweza. Naye Mola wangu Mlezi amekusanya ilimu ya vitu vyote, na hao miungu yenu haina chochote inacho jua! Je, mmeghafilika na yote hayo, na hamtambui kuwa mjinga aliye emewa hastahiki kuabudiwa?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Watu wake walimjadili kuhusu kumpwekesha Allah Mtukufu, Aliyetukuka, akasema «Mwanijadili juu ya kumpwekesha kwangu Allah Mtukufu kwa ibada, na hali Yeye Ameniongoza nikaujua upweke Wake? Na iwapo nyinyi mnanitisha na waungu wenu wasije wakanidhuru, basi mimi siwaogopi na hawatanidhuru isipokuwa Mola wangu Atake jambo. Mola wangu Ameenea kila kitu kwa ujuzi. Basi hamkumbuki mkajua kuwa Yeye, Peke Yake, Ndiye Mstahiki wa kuabudiwa?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net