Al-An'aam 6:79
الأنعامإِنِّى وَجَّهْتُ وَجْهِىَ لِلَّذِى فَطَرَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ حَنِيفًا ۖ وَمَآ أَنَا۠ مِنَ ٱلْمُشْرِكِينَ
Hakika mimi nimeuelekeza uso wangu kwa yule aliyeziumba mbingu na ardhi, huku nikiwa mnyoofu, wala mimi si miongoni mwa washirikina.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika mimi nimeuelekeza uso wangu sawa sawa kwa aliye ziumba mbingu na ardhi, wala mimi si miongoni mwa washirikina. [79]
[79] Alipo kwisha ona udhaifu wa viumbe alimuelekea aliye viumba, akisema: Mimi nimeyaelekeza makusudio yangu kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu pekee, ambaye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi. Nimejitenga na kila njia isipo kuwa Njia yake Yeye tu. Wala mimi, baada ya nilivyo kwisha ona dalili za Tawhidi (Umoja wa Allah), si katika wanao ridhia kuwa miongoni mwa washirikina kama wao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
«Mimi nimeelekea kwa uso wangu, katika ibada, kwa Allah Mtukufu, Aliyeshinda na kutukuka, Peke Yake, kwani Yeye Ndiye Aliyeumba mbingu na ardhi, nikiwa kando na ushirikina na nikielekea kwenye kumpwekesha Allah Mtukufu. Na mimi sikuwa ni miongoni mwa wenye kuwashirikisha wengine pamoja na Allah Mtukufu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net