Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 78

Al-An'aam 6:78

الأنعام

فَلَمَّا رَءَا ٱلشَّمْسَ بَازِغَةً قَالَ هَـٰذَا رَبِّى هَـٰذَآ أَكْبَرُ ۖ فَلَمَّآ أَفَلَتْ قَالَ يَـٰقَوْمِ إِنِّى بَرِىٓءٌ مِّمَّا تُشْرِكُونَ

Maana

Na alipoliona jua linachomoza, akasema: 'Huyu ndiye Mola wangu Mlezi. Huyu ni mkubwa zaidi.' Na lilipotua, akasema: Enyi kaumu yangu! Mimi niko mbali sana na hayo mnayoshirikisha.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na alipo liona jua linachomoza akasema: Huyu ndiye Mola Mlezi wangu. Huyu mkubwa kuliko wote. Lilipo tua, alisema: Enyi watu wangu! Mimi simo katika hayo mnayo fanyia ushirikina. [78]

[78] Tena baada ya hayo, akaliona jua linachomoza. Akasema: Huyu ndiye Mola Mlezi wangu, kwani huyu ni mkubwa kuliko nyota zinavyo onekana. Lilipo kuchwa, likapotea, akasema: Enyi watu wangu! Mimi simo katika kumshirikisha kwenu Mwenyezi Mungu na masanamu kwa kuyaabudu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Alipoliona jua limechomoza, alisema kuwaambia watu wake, «Hili ni mola wangu, hili ni kubwa kuliko nyota na mwezi.» Lilipozama, alisema kuwaambia watu wake, «Mimi nimejiepusha na ushirikina mulionao wa kuabudu mizimu, nyota na masanamu mnayoabudu badala ya Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net