Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 77

Al-An'aam 6:77

الأنعام

فَلَمَّا رَءَا ٱلْقَمَرَ بَازِغًا قَالَ هَـٰذَا رَبِّى ۖ فَلَمَّآ أَفَلَ قَالَ لَئِن لَّمْ يَهْدِنِى رَبِّى لَأَكُونَنَّ مِنَ ٱلْقَوْمِ ٱلضَّآلِّينَ

Maana

Alipouona mwezi unachomoza alisema: Huyu ndiye Mola wangu Mlezi. Na ulipotua, akasema: Kama Mola wangu Mlezi hataniongoa, basi hakika nitakuwa miongoni mwa kaumu waliopotea.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Alipo uona mwezi unachomoza alisema: Huyu ndiye Mola Mlezi wangu. Ulipotua akasema: Kama Mola Mlezi wangu hakuniongoa, nitakuwa katika kaumu walio potea. [77]

[77] Alipo uona mwezi umechomoza baada ya hayo, akasema akijiambia mwenyewe: Huyu ndiye Mola wangu Mlezi. Ulipo ondoka mwezi, na kukadhihiri kuvunjika ungu wake, akasema ili kuzielekeza nafsi zao ziombe hidaya: Ninaapa, kama Mola Mlezi wangu hakunihidi kwenye Haki, basi hapana shaka nitakuwa katika watu wanao babaika, (wasio jua mojapo la kulishika).

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ibrãhîm alipouona mwezi umechomoza alisema kuwaambia watu wake kwa njia ya kumvuta mtesi, «Huu ni mola wangu.» Ulipozama, alisema, akiwa ahitajia uongofu wa Mola wake, «Asiponiongoza Mola wangu kwenye usawa juu ya kumpwekesha Yeye nitakuwa ni miongoni mwa watu waliopotea njia ya sawa kwa kumuabudu asiyekuwa Allah Mtukufu».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net