Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 76

Al-An'aam 6:76

الأنعام

فَلَمَّا جَنَّ عَلَيْهِ ٱلَّيْلُ رَءَا كَوْكَبًا ۖ قَالَ هَـٰذَا رَبِّى ۖ فَلَمَّآ أَفَلَ قَالَ لَآ أُحِبُّ ٱلْـَٔافِلِينَ

Maana

Na ulipomwingilia usiku, aliona nyota kubwa, akasema: Huyu ndiye Mola wangu Mlezi. Na ilipotua, akasema: Siwapendi wanaotua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ulipo muingilia usiku akiona nyota, akasema: Huyu ni Mola Mlezi wangu. Ilipo tua akasema: Siwapendi wanao tua. [76]

[76] Ibrahim alimwomba Mola wake Mlezi, naye Mwenyezi Mungu akamhidi. Usiku ulipo kuja ukauziba mchana kwa kiza chake, akaona nyota inameremeta. Akasema: Huyu ndiye Mola wangu Mlezi. Ilipo potea, akasema kwa kuukataa ungu wa nyota: Sikubali kuabudu miungu inayo ondoka na kugeuka!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Giza la usiku lilipomuingilia Ibrãhîm, amani imshukiye, na kumfunika, alijadiliana na watu wake ili kuwathibitishia kuwa dini yao ni ya urongo. Na wao walikuwa wakiabudu nyota. Ibrãhîm, amani imshukie, aliona nyota, akasema, akiwavuta watu wake, ili awathibitishie tawhîd (upweke wa Allah Mtukufu) kihoja, «Hii ni mola wangu.» Nyota ilipozama alisema, «Mimi siwapendi waungu wanaozama».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net