Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 75

Al-An'aam 6:75

الأنعام

وَكَذَٰلِكَ نُرِىٓ إِبْرَٰهِيمَ مَلَكُوتَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَلِيَكُونَ مِنَ ٱلْمُوقِنِينَ

Maana

Na vivyo hivyo tulimwonyesha Ibrahim ufalme wa mbingu na ardhi, na ili awe miongoni mwa wenye yakini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kadhaalika tulimwonyesha Ibrahim ufalme wa mbingu na ardhi, na ili awe miongoni mwa wenye yakini. [75]

[75] Kama alivyo ona Ibrahim - kwa tawfiqi yetu - upotovu wa watu wake katika kuyafanya masanamu ndio miungu, kadhaalika tumemwonyesha ufalme wetu mkubwa wa mbinguni na duniani na viliomo humo, ili aweze kusimamisha hoja kwa watu wake, na ili azidi kuamini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kama tulivyomuongoza Ibrãhîm, amani imshukiye, kwenye haki katika jambo la ibada, tunamuonesha ufalme mkubwa unaokusanya mbingu na ardhi na uwezo wenye kushinda, ili awe miongoni mwa wenye kuzama katika Imani.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net