Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 74

Al-An'aam 6:74

الأنعام

وَإِذْ قَالَ إِبْرَٰهِيمُ لِأَبِيهِ ءَازَرَ أَتَتَّخِذُ أَصْنَامًا ءَالِهَةً ۖ إِنِّىٓ أَرَىٰكَ وَقَوْمَكَ فِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ

Maana

Na pale Ibrahim alipomwambia baba yake, Azar: Unayafanya masanamu kuwa ni miungu? Hakika mimi nakuona wewe na watu wako mko katika upotovu ulio wazi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na pale Ibrahim alipo mwambia baba yake, Azar: Unayafanya masanamu kuwa ni miungu? Hakika mimi nakuona wewe na watu wako mmo katika opotofu ulio wazi. [74]

[74] Na ewe Nabii! Kumbuka yaliyo kuwa pale Ibrahim alipo mwambia baba yake, Azar, naye ameudhika naye kwa kuwaabudu asiye kuwa Mwenyezi Mungu: Haikufalii wewe kuyafanya masanamu kuwa ni miungu. Hakika mimi nakuona wewe na kaumu yako walio nawe katika ibada hii, ni dhaahiri kuwa mko mbali na Njia ya Haki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kumbuka, ewe Mtume, mahujiano ya Ibrãhîm, amani imshukiye, na baba yake Ãzar. Ibrãhîm alipomwambia, «Je, unawafanya masanamu ni waungu, unawaabudu badala ya Allah Mtukufu? Mimi nakuona wewe na watu wako mko kwenye upotevu uliyo wazi, mko kando na njia ya haki».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net