Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 73

Al-An'aam 6:73

الأنعام

وَهُوَ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ بِٱلْحَقِّ ۖ وَيَوْمَ يَقُولُ كُن فَيَكُونُ ۚ قَوْلُهُ ٱلْحَقُّ ۚ وَلَهُ ٱلْمُلْكُ يَوْمَ يُنفَخُ فِى ٱلصُّورِ ۚ عَـٰلِمُ ٱلْغَيْبِ وَٱلشَّهَـٰدَةِ ۚ وَهُوَ ٱلْحَكِيمُ ٱلْخَبِيرُ

Maana

Naye ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi kwa Haki. Siku atakaposema: "Kuwa!" Na yawe. Kauli yake ni Haki. Na ufalme wote ni wake Siku litakapopulizwa barugumu, Mjuzi wa yaliyofichikana na yanayoonekana. Naye ndiye Mwenye hekima, Mwenye habari zote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Naye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi kwa Haki. Na anaposema: Kuwa! Basi huwa. Kauli yake ni Haki. Na ufalme wote ni wake Siku litapo pulizwa barugumu, Mjuzi wa yaliyo fichikana na yanayo onekana. Naye ndiye Mwenye hikima na Mwenye khabari. [73]

[73] Na ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi, na akasimamia uumbaji wake kwa Haki na hikima. Na wakati wowote Mwenyezi Mungu akitaka kiwe kitu kinakuwa papo hapo. Vitu huwa kwa neno: "Kuwa". Na kila neno lake ni la kweli na la haki. Na Yeye peke yake ndiye Mwenye uweza wa kutenda usio na ukomo Siku ya Kiyama, siku litapo pulizwa barugumu la kutangazwa ufufuo. Naye, Subhanahu, ndiye Mwenye kutulia juu ya ujuzi wake wa mambo yaliyo fichikana na yanayo onekana. Na ndiye anaye endesha mambo yake yote kwa hikima, na ndiye Mwenye kukusanya katika ujuzi wake mambo yaliyo fichikana na mambo yaliyo dhihiri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Allah Mtukufu, kutakasika na sifa pungufu ni Kwake, Ndiye Aliyeumba mbingu na ardhi kwa haki. Na taja,ewe Mtume, Atakaposema Allah Mtukufu Siku ya Kiyama, «Kuwa» na ikawa kulingana na amri Yake, kama kupepesa macho au muda mfupi zaidi. Neno lake Ndio haki iliokamilika. Na ni Wake ufalme, Peke Yake, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Siku Malaika atakapopuzia Parapanda, mpuzio wa pili ambao, kwa huo, roho zitarudi kwenye miili. Na Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni kwake, Ndiye Anayeyajua yaliyofichika na hisi zenu, enyi watu, mnayoyaona kwa macho yenu. Yeye Ndiye Mwenye hekima, Anayeweka mambo mahali pake, Mtambuzi wa mambo ya viumbe Vyake. Na Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Ndiye Anayehusika na mambo haya na mengineyo, mwanzo na mwisho, kuanzisha kuumba na ukomo wake. Na Yeye, Peke Yake, Ndiye Ambaye inapasa kwa waja kufuata sheria Yake, kujisalimisha kwa hukumu Yake na kuwa nahamu ya kupata radhi Zake na msamaha Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net