Al-An'aam
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَهُوَ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ بِٱلْحَقِّ ۖ وَيَوْمَ يَقُولُ كُن فَيَكُونُ ۚ قَوْلُهُ ٱلْحَقُّ ۚ وَلَهُ ٱلْمُلْكُ يَوْمَ يُنفَخُ فِى ٱلصُّورِ ۚ عَـٰلِمُ ٱلْغَيْبِ وَٱلشَّهَـٰدَةِ ۚ وَهُوَ ٱلْحَكِيمُ ٱلْخَبِيرُ 73
{73} "Naye ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi kwa Haki," ili awaamrishe waja wake na awakataze, na awalipe mazuri na awaadhibu, "Na siku atakaposema: Kuwa! Basi likawa. Kauli yake ni Haki." Ambayo haina shaka yoyote juu yake wala uwili, na wala hasemi kitu bure. "Na wake ufalme wote Siku litapopulizwa katika barugumu." Yaani, Siku ya Qiyaama Atampwekesha kwa ukumbusho ingawa Yeye ndiye Mwenye kila kitu. Kwa sababu mali zimekatiliwa mbali ndani yake, basi hakuna mfalme aliyesalia isipokuwa Mungu Mmoja, Mwenye Nguvu Zote. "Mwenye kuyajua vyema ya ghaibu na yanayoonekana. Naye ndiye Mwenye hekima kubwa, Mwenye habari zote." Yeye ndiye Mwenye hekima kamili, na neema nyingi, na fadhila kubwa, na elimu inayojumuisha siri, na mambo ya ndani na yaliyofichika. Hakuna mungu isipokuwa Yeye, na hakuna Mola Mlezi mwingine isipokuwa Yeye.