Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-An'aam
Sura ya 6

Al-An'aam

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 74

وَإِذْ قَالَ إِبْرَٰهِيمُ لِأَبِيهِ ءَازَرَ أَتَتَّخِذُ أَصْنَامًا ءَالِهَةً ۖ إِنِّىٓ أَرَىٰكَ وَقَوْمَكَ فِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ 74

{74} Yeye Mtukufu Anasema, Kikumbuke kisa cha Ibrahim, amani iwe juu yake, ukimsifu na kumtukuza katika hali alipolingania tauhidi na kukataza kwake ushirikina. "Pale Ibrahim alipomwambia baba yake, Azar: Je, unayafanya masanamu kuwa ni miungu?" Yaani, hayanufaishi wala hayadhuru, na wala hayana kitu katika jambo hilo. "Hakika mimi nakuona wewe na kaumu yako mmo katika opotofu ulio wazi," pale mlipowaabudu kile kisichostahiki chochote katika ibada, na kumuacha kwenu kumwabudu Muumba wenu, na Mwenye kuwaruzuku, na Mwenye kuwaendesha.