Al-An'aam 6:72
الأنعاموَأَنْ أَقِيمُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَٱتَّقُوهُ ۚ وَهُوَ ٱلَّذِىٓ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ
Na mshike Sala, na mcheni Yeye, na kwake Yeye ndiko mtakakokusanywa
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mshike Swala, na mcheni Yeye, na kwake Yeye ndiko mtako kusanywa. [72]
[72] Waachilieni mbali hao washirikina baada ya kuwa mmewaita kwenye uwongofu, na nendeni kwenye ibada ya Mola wenu Mlezi. Na timizeni SWala kwa njia ya unyenyekevu ulio kamilika kabisa. Na mkhofuni Mwenyezi Mungu, na timizeni amri zake. Kwani kwake Yeye ndio mtakusanywa nyote nyinyi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hivyohivyo tumeamrishwa tusimamishe Swala kikamilifu, tumuogope Yeye kwa kufanya maamrisho Yake na kuepuka makatazo Yake. Na Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu, Ndiye Ambaye Kwake Yeye watakusanywa viumbe wote Siku ya Kiyama.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net