Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 71

Al-An'aam 6:71

الأنعام

قُلْ أَنَدْعُوا۟ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَنفَعُنَا وَلَا يَضُرُّنَا وَنُرَدُّ عَلَىٰٓ أَعْقَابِنَا بَعْدَ إِذْ هَدَىٰنَا ٱللَّهُ كَٱلَّذِى ٱسْتَهْوَتْهُ ٱلشَّيَـٰطِينُ فِى ٱلْأَرْضِ حَيْرَانَ لَهُۥٓ أَصْحَـٰبٌ يَدْعُونَهُۥٓ إِلَى ٱلْهُدَى ٱئْتِنَا ۗ قُلْ إِنَّ هُدَى ٱللَّهِ هُوَ ٱلْهُدَىٰ ۖ وَأُمِرْنَا لِنُسْلِمَ لِرَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ

Maana

Sema: Je, tumuombe asiyekuwa Mwenyezi Mungu ambaye hatufai wala hatudhuru, na turejee nyuma baada ya Mwenyezi Mungu kwisha tuongoa? Tuwe kama ambao mashetani wamempumbaza katika ardhi, amechanganyikiwa? Anao marafiki wanaomwita aende kwenye uwongofu, wakimwambia: 'Njoo kwetu!' Sema: Hakika uongofu wa Mwenyezi Mungu ndio Uongofu. Nasi tumeamrishwa tusilimu kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Je, tumuombe asiye kuwa Mwenyezi Mungu ambae hatufai wala hatudhuru, na turejee nyuma baada ya Mwenyezi Mungu kwisha tuhidi? Tuwe kama ambao mashet'ani wamempumbaza katika ardhi, amebabaika? Anao marafiki wanao mwita ende kwenye uwongofu, wakimwambia: Njoo kwetu! Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio Uwongofu. Nasi tumeamrishwa tusilimu kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote, [71]

[71] Waambie hawa makafiri kwa kuwasibabi: Je, inasihi kuwa tumuabudu asiye kuwa Mwenyezi Mungu, asiye weza kutuletea nafuu wala dhara? Na turejee kwenye shirki baada ya kuwa Mwenyezi Mungu kesha tupa tawfiqi ya kufikia Imani? Na tuwe kama aliye zugwa na mashetani na wakampoteza katika ardhi, akawa yuko katika pweleo lisilo weza kumwongoa kufuata Njia iliyo nyooka, na hali anao marafiki walio ongoka nao wanajaribu kumwokoa atoke kwenye upotofu, huku wakisema: Rejea kwenye njia yetu iliyo sawa; naye akawa hawaitikii!! Sema ewe Nabii: Hakika Uislamu ndio uwongofu na ndio uwongozi, na vyenginevyo ni upotofu tu. Na Mwenyezi Mungu ametuamrisha tuufuate Uislamu. Naye ndiye Muumba wa viumbe vyote, na ndiye Mwenye kuviruzuku, na Mwenye kupanga mambo yao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Je, tuabudu, asiyekuwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, masanamu yasionufaisha wala kudhuru? Je, turudi ukafirini baada ya Allah Mtukufu kutuongoza kwenye Uislamu, tukafanana, katika kurudi kwetu ukafirini, na aliyeharibika akili yake kwa kusawazwa na mashetani akapotea njia ardhini na hali yeye ana marafiki wenye akili, wenye Imani, wamwita kwenye njia ya sawa ambayo wao wako akawa anakataa?» Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Uongofu wa Allah Mtukufu Aliyenituma mimi ndio uongofu wa haki. Na sote tumeamrishwa tujisalimishe kwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Bwana wa viumbe vyote, kwa kumuabudu, Peke Yake, Asiye na mshirika, kwani Yeye Ndiye Mola na Mmiliki wa kila kitu».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net