Al-An'aam 6:70
الأنعاموَذَرِ ٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُوا۟ دِينَهُمْ لَعِبًا وَلَهْوًا وَغَرَّتْهُمُ ٱلْحَيَوٰةُ ٱلدُّنْيَا ۚ وَذَكِّرْ بِهِۦٓ أَن تُبْسَلَ نَفْسٌۢ بِمَا كَسَبَتْ لَيْسَ لَهَا مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلِىٌّ وَلَا شَفِيعٌ وَإِن تَعْدِلْ كُلَّ عَدْلٍ لَّا يُؤْخَذْ مِنْهَآ ۗ أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ أُبْسِلُوا۟ بِمَا كَسَبُوا۟ ۖ لَهُمْ شَرَابٌ مِّنْ حَمِيمٍ وَعَذَابٌ أَلِيمٌۢ بِمَا كَانُوا۟ يَكْفُرُونَ
Waachilie mbali walioifanya dini yao ni mchezo na pumbao, na uhai wa dunia ukawadanganya. Nawe kumbusha kwayo, isije nafsi ikaangamizwa kwa sababu ya iliyoyachuma, nayo haina mlinzi wala mwombezi ila Mwenyezi Mungu. Na ingetoa kila fidia, haitokubaliwa. Hao ndio walioangamizwa kwa sababu ya yale waliyoyachuma. Wao watapata kinywaji cha maji ya moto kabisa, na adhabu chungu kwa sababu ya walivyokuwa wakikufuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Waachilie mbali walio ifanya dini yao ni mchezo na pumbao, na uhai wa dunia ukawaghuri. Nawe kumbusha kwayo, isije nafsi ikaangamizwa kwa sababu ya iliyo yachuma, nayo haina mlinzi wala mwombezi ila Mwenyezi Mungu. Na ingatoa kila fidia haitokubaliwa. Hao ndio walio angamizwa kwa sababu ya yale waliyo yachuma. Wao watapata kinywaji cha maji ya moto kabisa, na adhabu chungu. [70]
[70] Na ewe Nabii, waachilie mbali wale walio fanya sharia yao, mwendo wao, pumbao na mchezo, na wakakhadaika na maisha ya dunia wakaacha ya Akhera. Na daima kumbusha kwa Qur'ani, na wahadharishe vitisho vya Siku ambayo nafsi itafungika na a'mali yake, itapo kuwa hapana wa kunusuru wala wa kusaidia isipo kuwa Mwenyezi Mungu. Na kila fidia ya kujiokoa haitokubaliwa. Hao makafiri watafungwa katika adhabu kwa sababu ya shari waliyo itenda. Katika Jahannamu watapewa kinywaji kimoto mwisho wa umoto, na adhabu chungu mno kwa sababu ya kufuru zao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na waache, ewe Mtume, hawa washirikina ambao wameifanya dini ya Uislamu ni mchezo na pumbao, wazifanyia shere aya za Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na yamewaghuri wao maisha ya kilimwengu pamoja na pambo lake. Na wakumbushe, kwa Qur’ani, hawa washirikina na wengineo, ili nafsi isifungike kwa madhambi yake na kumkanusha kwake Mola wake. Haina, isipokuwa Allah Mtukufu, mlinzi mwenye kuinusuru akaiokoa na adhabu Yake, wala muombezi mwenye kuiombea mbele Yake. Na ikitoa ili kujikomboa kiwango kiwacho cha fidia haitakubaliwa kwake. Hao ndio ambao wamefungika na dhambi zao. Watakuwa na kinywaji moto sana na adhabu yenye kuumiza Motoni, kwa sababu ya kumkanusha kwao Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Mtume Wake, Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie,) na dini ya Uislamu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net